Agano la Kale

Agano Jipya

Wafilipi 4:12-23 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa.

13. Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu.

14. Hata hivyo, nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana nami katika taabu zangu.

15. Nyinyi Wafilipi mwafahamu wenyewe kwamba mwanzoni mwa kuhubiri Habari Njema, nilipokuwa naondoka Makedonia, nyinyi peke yenu ndio kanisa lililonisaidia; nyinyi peke yenu ndio mlioshirikiana nami katika kupokea na kuwapa wengine mahitaji.

16. Nilipokuwa nahitaji msaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidi ya mara moja.

17. Sio kwamba napenda tu kupokea zawadi; ninachotaka ni faida iongezwe katika hazina yenu.

18. Basi, nimekwisha pokea vitu vyote mlivyonipa, tena ni zaidi kuliko nilivyohitaji. Nina kila kitu kwa vile sasa Epafrodito amekwisha niletea zawadi zenu. Zawadi hizi ni kama tambiko yenye harufu nzuri, sadaka inayokubaliwa na kumpendeza Mungu.

19. Basi, Mungu wangu, kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo, atawapeni mahitaji yenu yote.

20. Utukufu uwe kwa Mungu wetu na Baba yetu, milele na milele. Amina.

21. Nawasalimu watu wote wa Mungu walio wake Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami hapa wanawasalimuni.

22. Watu wote wa Mungu hapa, na hasa wale walio katika ikulu ya mfalme, wanawasalimuni.

23. Nawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Kusoma sura kamili Wafilipi 4