Agano la Kale

Agano Jipya

Waefeso 5:2-13 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Upendo uongoze maisha yenu kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama tambiko yenye harufu nzuri na sadaka impendezayo Mungu.

3. Kwa vile nyinyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu.

4. Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa.

5. Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mchoyo, (ambao ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.

6. Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii.

7. Basi, msishirikiane nao.

8. Zamani nyinyi mlikuwa gizani, lakini sasa nyinyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga,

9. maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli.

10. Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana.

11. Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni.

12. Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja.

13. Lakini kila kitu kikifichuliwa na mwanga, ukweli wake hudhihirishwa;

Kusoma sura kamili Waefeso 5