Agano la Kale

Agano Jipya

Ufunuo 22:18-21 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Mimi Yohane nawapa onyo wote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: Mtu yeyote akiongeza chochote katika mambo haya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

19. Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uhai, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki.

20. Naye anayetoa ushahidi wake juu ya mambo haya asema: “Kweli naja upesi.”Amina. Njoo Bwana Yesu!

21. Nawatakieni nyote neema ya Bwana Yesu. Amina.

Kusoma sura kamili Ufunuo 22