Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 26:16-26 Biblia Habari Njema (BHN)

16. na tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti.

17. Siku ya kwanza kabla ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”

18. Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mwanamume fulani, mkamwambie: ‘Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.’”

19. Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaandaa Pasaka.

20. Kulipokuwa jioni, Yesu akakaa mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.

21. Walipokuwa wakila, Yesu akasema, “Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti.”

22. Wanafunzi wakahuzunika sana, wakaanza kuuliza mmojammoja, “Bwana! Je, ni mimi?”

23. Yesu akajibu, “Anayechovya mkate pamoja nami katika bakuli ndiye atakayenisaliti.

24. Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa.”

25. Yuda, ambaye ndiye aliyetaka kumsaliti, akamwuliza, “Mwalimu! Je, ni mimi?” Yesu akamjibu, “Wewe umesema.”

26. Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akamshukuru Mungu, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, “Twaeni mle; huu ni mwili wangu.”

Kusoma sura kamili Mathayo 26