Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 21:34-43 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Wakati wa mavuno ulipofika, aliwatuma watumishi wake kwa wale wakulima, ili wakachukue sehemu ya mavuno yake.

35. Wale wakulima wakawakamata hao watumishi; mmoja wakampiga, mwingine wakamuua na mwingine wakampiga mawe.

36. Huyo mtu akawatuma tena watumishi wengine, wengi kuliko wa safari ya kwanza. Wale wakulima wakawatendea namna ileile.

37. Mwishowe akamtuma mwanawe huku akifikiri: ‘Watamjali mwanangu.’

38. Lakini wale wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa wao: ‘Huyu ndiye mrithi; na tumuue ili tuuchukue urithi wake!’

39. Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua.

40. “Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje hao wakulima?”

41. Wao wakamjibu, “Atawaangamiza vibaya hao waovu, na lile shamba atawapa wakulima wengine ambao watampa sehemu ya mavuno wakati wake.”

42. Hapo Yesu akawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu?‘Jiwe walilokataa waashisasa limekuwa jiwe kuu la msingi.Bwana ndiye aliyefanya jambo hili,nalo ni la ajabu sana kwetu!’

43. “Kwa hiyo nawaambieni, ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wa mataifa mengine wenye kutoa matunda yake.”

Kusoma sura kamili Mathayo 21