Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 14:12-19 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.

13. Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini.

14. Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.

15. Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”

16. Yesu akawaambia, “Si lazima waende, wapeni nyinyi chakula.”

17. Lakini wao wakamwambia, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili.”

18. Yesu akawaambia, “Nileteeni hapa.”

19. Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.

Kusoma sura kamili Mathayo 14