Agano la Kale

Agano Jipya

Matendo 2:8-19 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Imekuwaje, basi, kwamba kila mmoja wetu anawasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe?

9. Baadhi yetu ni Waparthi, Wamedi na Waelamu; wengine ni wenyeji wa Mesopotamia, Yudea, Kapadokia, Ponto na Asia,

10. Frugia na Pamfulia, Misri na sehemu za Libia karibu na Kurene; wengine wetu ni wageni kutoka Roma,

11. Wayahudi na watu walioongokea dini ya Kiyahudi; wengine wametoka Krete na Arabia. Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetu wenyewe mambo makuu ya Mungu.”

12. Wote walishangaa na kufadhaika huku wakiulizana, “Hii ina maana gani?”

13. Lakini wengine wakawadhihaki wakisema, “Watu hawa wamelewa divai mpya!”

14. Lakini Petro alisimama pamoja na wale kumi na mmoja akaanza kuwahutubia watu kwa sauti kubwa: “Ndugu Wayahudi nanyi nyote mnaokaa hapa Yerusalemu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.

15. Watu hawa hawakulewa kama mnavyodhani; mbona ni saa tatu tu asubuhi?

16. Ukweli ni kwamba jambo hili ni lile alilosema nabii Yoeli:

17. ‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana,nitawamiminia binadamu wote Roho wangu.Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii,vijana wenu wataona maono,na wazee wenu wataota ndoto.

18. Naam, hata watumishi wangu wa kiume na kike,nitawamiminia Roho wangu siku zile,nao watatoa unabii.

19. Nitatenda miujiza juu angani,na ishara chini duniani;kutakuwa na damu, moto na moshi mzito;

Kusoma sura kamili Matendo 2