Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 12:15-25 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.”

16. Wakamwonesha. Naye akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.”

17. Basi, Yesu akawaambia, “Ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.” Wakashangazwa sana naye.

18. Masadukayo ambao husema kwamba hakuna ufufuo walimwendea Yesu, wakamwuliza,

19. “Mwalimu, Mose alituagiza hivi: ‘Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.’

20. Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.

21. Ndugu wa pili akamwoa huyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto; na ndugu watatu hali kadhalika.

22. Wote saba walikufa bila kuacha mtoto. Mwishowe yule mama mjane naye akafa.

23. Basi, siku watu watakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wa nani? Wote saba walikuwa wamemwoa.”

24. Yesu akawaambia, “Nyinyi mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu.

25. Maana wafu watakapofufuka hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni.

Kusoma sura kamili Marko 12