Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 20:35-47 Biblia Habari Njema (BHN)

35. lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa.

36. Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.

37. Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.

38. Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana kwake wote wanaishi.”

39. Baadhi ya wale waalimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umejibu vema kabisa.”

40. Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.

41. Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?

42. Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi:‘Bwana alimwambia Bwana wangu:Keti upande wangu wa kulia

43. mpaka niwaweke maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.’

44. Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?”

45. Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote,

46. “Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.

47. Huwadhulumu wajane huku wakisingizia kuwa wema kwa kusali sala ndefu. Hao watapata hukumu kali zaidi!”

Kusoma sura kamili Luka 20