Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 20:31-41 Biblia Habari Njema (BHN)

31. na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba – wote walikufa bila kuacha watoto.

32. Mwishowe akafa pia yule mwanamke.

33. Je, siku wafu watakapofufuliwa, mama huyo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.”

34. Yesu akawaambia, “Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa;

35. lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa.

36. Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.

37. Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.

38. Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana kwake wote wanaishi.”

39. Baadhi ya wale waalimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umejibu vema kabisa.”

40. Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.

41. Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?

Kusoma sura kamili Luka 20