Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 20:10-17 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo, wakamrudisha mikono mitupu.

11. Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.

12. Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza.

13. Yule mwenye shamba akafikiri: ‘Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi; labda watamjali yeye.’

14. Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: ‘Huyu ndiye mrithi. Basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu.’

15. Basi, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua.” Yesu akauliza, “Yule mwenye shamba atawafanya nini hao wakulima?

16. Atakuja kuwaangamiza wakulima hao, na kuwapa wakulima wengine hilo shamba la mizabibu.” Watu waliposikia maneno hayo, walisema: “Hasha! Yasitukie hata kidogo!”

17. Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Maandiko haya Matakatifu yana maana gani, basi?‘Jiwe walilokataa waashi,sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!’

Kusoma sura kamili Luka 20