Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 17:12-25 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.

13. Wakapaza sauti wakisema, “Yesu Mwalimu, tuonee huruma!”

14. Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajioneshe kwa makuhani.” Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.

15. Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa, alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.

16. Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.

17. Hapo Yesu akasema, “Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?

18. Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?”

19. Halafu akamwambia huyo mtu, “Simama, uende zako; imani yako imekuponya.”

20. Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, “Ufalme wa Mungu utakuja lini?” Naye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.

21. Wala hakuna atakayeweza kusema, ‘Uko hapa’, au ‘Uko pale’. Kwa kweli ufalme wa Mungu uko kati yenu.”

22. Halafu akawaambia wanafunzi wake, “Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.

23. Na watu watawaambieni: ‘Tazameni, yuko pale!’ Au ‘Tazameni, yupo hapa!’ Lakini nyinyi msitoke wala msiwafuate.

24. Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku ile yake.

25. Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.

Kusoma sura kamili Luka 17