Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 15:16-27 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu.

17. Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?

18. Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia.

19. Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’

20. Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.

21. “Mwanae akamwambia: ‘Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.’

22. Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: ‘Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!

23. Mchinjeni ndama mnono; tule na kusherehekea!

24. Kwa sababu huyu mwanangu; alikuwa amekufa, kumbe yu hai; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’ Wakaanza kufanya sherehe.

25. “Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani, akasikia vifijo na ngoma.

26. Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: ‘Kuna nini?’

27. Huyo mtumishi akamwambia: ‘Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.’

Kusoma sura kamili Luka 15