1. Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akisali. Alipomaliza kusali, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tunakuomba utufundishe kusali kama Yohane Mbatizaji alivyowafundisha wanafunzi wake.”
2. Yesu akawaambia, “Mnaposali, semeni:‘Baba!Jina lako litukuzwe;ufalme wako ufike.
3. Utupe daima chakula chetu cha kila siku.
4. Utusamehe dhambi zetu,maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea;wala usitutie katika majaribu.’”
5. Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake usiku wa manane, akamwambia: ‘Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu,
6. kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha kumpa.’