Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wakorintho 2:3-8 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Ndiyo maana niliwaandikia: Sikutaka kuja kwenu na kuhuzunishwa na nyinyi ambao ndio mngepaswa kuwa furaha yangu. Nina hakika kwamba mimi nikifurahi, nyinyi nyote pia mnafurahi.

4. Nilipowaandikia hapo awali katika hali ya huzuni na sikitiko moyoni na kwa machozi mengi, haikuwa kwa ajili ya kuwahuzunisha nyinyi, bali kwa ajili ya kuwaonesheni kwamba nawapenda mno.

5. Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi, ila amewahuzunisha nyinyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.

6. Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengi wenu inamtosha.

7. Iliyobakia ni afadhali kwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyo ili asije akahuzunika mno na kukata tamaa kabisa.

8. Kwa hiyo nawasihi: Mwonesheni kwamba mnampenda.

Kusoma sura kamili 2 Wakorintho 2