Agano la Kale

Agano Jipya

1 Yohane 5:3-10 Biblia Habari Njema (BHN)

3. maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na, amri zake si ngumu,

4. maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu.

5. Nani, basi, awezaye kuushinda ulimwengu? Ni yule anayeamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

6. Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji ya ubatizo wake na kwa damu ya kifo chake. Hakuja kwa maji tu, bali kwa maji na kwa damu. Naye Roho anashuhudia kwamba ni kweli, kwani Roho ni ukweli.

7. Basi, wako mashahidi watatu:

8. Roho, maji na damu; na ushahidi wa hawa watatu waafikiana.

9. Ikiwa twaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; na huu ndio ushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu ya Mwanae.

10. Anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushahidi huo ndani yake; lakini asiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwa mwongo, maana hakuamini ushahidi alioutoa Mungu juu ya Mwanae.

Kusoma sura kamili 1 Yohane 5