Agano la Kale

Agano Jipya

1 Yohane 1:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Habari hii yahusu Neno la uhai lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe.

2. Uhai huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na kuwaambieni juu ya uhai huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu.

3. Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni nyinyi pia, ili nanyi mpate kushirikiana nasi katika umoja tulio nao na Baba na Mwanae Yesu Kristo.

4. Tunawaandikia nyinyi mambo haya kusudi furaha yetu ikamilike.

Kusoma sura kamili 1 Yohane 1