Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 16:4-16 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami.

5. Nitakuja kwenu baada ya kupitia Makedonia – maana nataraji kupitia Makedonia.

6. Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.

7. Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.

8. Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste.

9. Mlango uko wazi kabisa kwa ajili ya kazi yangu muhimu hapa, ingawa wapinzani nao ni wengi.

10. Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.

11. Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieni aendelee na safari yake kwa amani ili aweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamoja na ndugu zetu.

12. Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.

13. Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu.

14. Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo.

15. Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu. Ninawasihi nyinyi ndugu zangu,

16. muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumika pamoja nao.

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 16