Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4

Agano la Kale

Agano Jipya

Yon. 2 Swahili Union Version (SUV)

Wimbo wa Kushukuru

1. Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,

2. Akasema,Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu,Naye akaniitikia;Katika tumbo la kuzimu naliomba,Nawe ukasikia sauti yangu.

3. Maana ulinitupa vilindini,Ndani ya moyo wa bahari;Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.

4. Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.

5. Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;Vilindi vilinizunguka;Mwani ulikizinga kichwa changu;

6. Nalishuka hata pande za chini za milima;Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele;Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni,Ee BWANA, Mungu wangu,

7. Roho yangu ilipozimia ndani yangu,Nalimkumbuka BWANA;Maombi yangu yakakuwasilia,Katika hekalu lako takatifu.

8. Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongoHujitenga na rehema zao wenyewe;

9. Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;Nitaziondoa nadhiri zangu.Wokovu hutoka kwa BWANA.

10. BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.