Agano la Kale

Agano Jipya

Neh. 7:37-45 Swahili Union Version (SUV)

37. Wana wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na mmoja.

38. Watu wa Senaa, elfu tatu mia kenda na thelathini.

39. Makuhani; Wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu.

40. Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.

41. Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba.

42. Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.

43. Walawi; Wana wa Yeshua, wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne.

44. Waimbaji; Wana wa Asafu, mia moja arobaini na wanane.

45. Mabawabu; Wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, mia moja thelathini na wanane.

Kusoma sura kamili Neh. 7