Agano la Kale

Agano Jipya

Neh. 7:23-39 Swahili Union Version (SUV)

23. Wana wa Besai, mia tatu ishirini na wanne.

24. Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.

25. Wana wa Gibeoni, tisini na watano.

26. Watu wa Bethlehemu na Netofa, mia na themanini na wanane.

27. Watu wa Anathothi, mia na ishirini na wanane.

28. Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili.

29. Watu wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu.

30. Watu wa Rama na Geba, mia sita na ishirini na mmoja.

31. Watu wa Mikmashi, mia moja na ishirini na wawili.

32. Watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu.

33. Watu wa Nebo, hamsini na wawili.

34. Wana wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.

35. Wana wa Harimu, mia tatu na ishirini.

36. Wana wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano.

37. Wana wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na mmoja.

38. Watu wa Senaa, elfu tatu mia kenda na thelathini.

39. Makuhani; Wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu.

Kusoma sura kamili Neh. 7