Agano la Kale

Agano Jipya

Neh. 3:8-22 Swahili Union Version (SUV)

8. Na baada yao akafanyiza Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana.

9. Na baada yao akafanyiza Refaya, mwana wa Huri, akida wa nusu ya Yerusalemu.

10. Na baada yao akafanyiza Yedaya, mwana wa Harumafu, kuielekea nyumba yake. Na baada yake akafanyiza Hatushi, mwana wa Hashabneya.

11. Malkiya, mwana wa Harimu, na Hashubu, mwana wa Pahath-moabu, wakafanyiza sehemu nyingine, na mnara wa tanuu.

12. Na baada yake akafanyiza Shalumu, mwana wa Haloheshi, akida wa nusu ya Yerusalemu, yeye na binti zake.

13. Lango la bondeni wakalifanyiza Hanuni, nao wakaao Zanoa; wakalijenga, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuta wa dhiraa elfu mpaka lango la jaa.

14. Na lango la jaa akalifanyiza Malkiya, mwana wa Rekabu, akida wa mtaa wa Beth-hakeremu; akalijenga, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.

15. Na lango la chemchemi akalifanyiza Shalumu, mwana wa Kolhoze, akida wa mtaa wa Mispa; akalijenga na kulifunika, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi.

16. Baada yake akafanyiza Nehemia, mwana wa Azbuki, akida wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya mashujaa.

17. Baada yake wakafanyiza Walawi, Rehumi, mwana wa Bani. Baada yake akafanyiza Hashabia, akida wa nusu ya mtaa wa Keila, kwa mtaa wake.

18. Baada yake wakafanyiza ndugu zao, Binui, mwana wa Henadadi, akida wa nusu ya mtaa wa Keila.

19. Na baada yake akafanyiza Ezeri, mwana wa Yeshua, akida wa Mispa, sehemu nyingine, kupaelekea penye kupanda kwa ghala ya silaha, ukuta ugeukapo.

20. Baada yake Baruki, mwana wa Zakai, akafanyiza kwa bidii sehemu nyingine, toka ugeukapo ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu.

21. Baada yake akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, sehemu nyingine, toka mlango wa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu.

22. Na baada yake wakafanyiza makuhani, watu wa Uwandani.

Kusoma sura kamili Neh. 3