Agano la Kale

Agano Jipya

Neh. 12:26-38 Swahili Union Version (SUV)

26. Hao walikuwapo siku za Yoyakimu, mwana ya Yoshua, mwana wa Yosadaki, na siku za Nehemia, liwali, na Ezra, kuhani, mwandishi.

27. Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, wapate kufanya wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi.

28. Waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya Yerusalemu, na kutoka vijiji vya Wanetofathi;

29. tena toka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi; kwa maana waimbaji hao walikuwa wamejijengea vijiji katika viunga vya Yerusalemu.

30. Makuhani na Walawi wakajitakasa, nao wakawatakasa watu, na malango, na ukuta.

31. Ndipo nikawapandisha wakuu wa Yuda juu ya ukuta, nikawaagiza mikutano mikubwa miwili ya hao walioshukuru, na kuandamana; mmoja uende kwa kuume ukutani kuliendea lango la jaa;

32. na baada yao wakaenda Hoshaya, na nusu ya wakuu wa Yuda,

33. na Azaria, na Ezra, na Meshulamu,

34. na Yuda, na Benyamini, na Shemaya, na Yeremia,

35. na baadhi ya makuhani wenye baragumu; Zekaria, mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu;

36. na ndugu zake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda, na Hanani, wenye vinanda vya Daudi mtu wa Mungu; Ezra, mwandishi, akawatangulia;

37. na kwa lango la chemchemi, wakienda moja kwa moja mbele yao, wakapanda madaraja ya mji wa Daudi, uinukapo ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, mpaka lango la maji upande wa mashariki.

38. Na mkutano wa pili wao wenye kushukuru wakaenda kuwalaki, na mimi nikafuata nyuma yao, pamoja na nusu ya watu, ukutani juu ya mnara wa tanuu, mpaka ule ukuta mpana;

Kusoma sura kamili Neh. 12