Agano la Kale

Agano Jipya

Mhu. 4:13-16 Swahili Union Version (SUV)

13. Heri kijana maskini mwenye hekimaKuliko mfalme mzee mpumbavu.ambaye hajui tena kupokea maonyo.

14. Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki; naam, hata katika ufalme wake alizaliwa hali ya umaskini.

15. Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana, huyo wa pili aliyesimama badala ya yule.

16. Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kujilisha upepo.

Kusoma sura kamili Mhu. 4