Agano la Kale

Agano Jipya

Mhu. 1:1-10 Swahili Union Version (SUV)

1. Maneno ya Mhubiri, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu

2. Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.

3. Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?

4. Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.

5. Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.

6. Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.

7. Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.

8. Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.

9. Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.

10. Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.

Kusoma sura kamili Mhu. 1