Agano la Kale

Agano Jipya

Kum. 23:2-9 Swahili Union Version (SUV)

2. Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa BWANA.

3. Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa BWANA; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa BWANA milele;

4. kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize.

5. Lakini BWANA, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; BWANA, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda BWANA, Mungu wako.

6. Usitafute amani yao wala heri yao siku zako zote, milele.

7. Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake.

8. Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa BWANA.

9. Utakapotoka kwenda juu ya adui zako nawe u katika marago, jilinde na kila neno baya.

Kusoma sura kamili Kum. 23