Agano la Kale

Agano Jipya

Amo. 7:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme.

2. Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.

3. BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.

Kusoma sura kamili Amo. 7