Agano la Kale

Agano Jipya

Amo. 5:2-7 Swahili Union Version (SUV)

2. Bikira wa Israeli ameanguka;hatainuka tena;Ameangushwa katika nchi yake;hakuna mtu wa kumwinua.

3. Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu, utasaziwa watu mia, na mji uliotoka wenye watu mia, utasaziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli.

4. Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi;

5. bali msitafute Betheli, wala msiingie Gilgali, wala msipite kwenda Beer-sheba; kwani Gilgali hakika yake itakwenda utumwani, na Betheli itakuwa ubatili.

6. Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli.

7. Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini,

Kusoma sura kamili Amo. 5