Agano la Kale

Agano Jipya

Amo. 1:13-15 Swahili Union Version (SUV)

13. Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;

14. lakini nitawasha moto katika ukuta wa Raba, nao utayateketeza majumba yake; pamoja na kupiga kelele siku ya vita, pamoja na tufani katika siku ya chamchela;

15. na mfalme wao atakwenda utumwani, yeye na wakuu wake wote pamoja, asema BWANA.

Kusoma sura kamili Amo. 1