Agano la Kale

Agano Jipya

Yud. 1:18-21 Swahili Union Version (SUV)

18. ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu.

19. Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.

20. Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,

21. jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.

Kusoma sura kamili Yud. 1