Agano la Kale

Agano Jipya

Yn. 9:34-41 Swahili Union Version (SUV)

34. Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.

35. Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?

36. Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?

37. Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.

38. Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.

39. Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.

40. Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?

41. Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.

Kusoma sura kamili Yn. 9