Agano la Kale

Agano Jipya

Yn. 7:40-48 Swahili Union Version (SUV)

40. Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.

41. Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya?

42. Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?

43. Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake.

44. Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.

45. Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?

46. Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena.

47. Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?

48. Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?

Kusoma sura kamili Yn. 7