Agano la Kale

Agano Jipya

Yn. 19:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi.

2. Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau.

3. Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi.

4. Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake.

5. Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu!

6. Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake.

7. Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.

8. Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa.

9. Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote.

Kusoma sura kamili Yn. 19