Agano la Kale

Agano Jipya

Yn. 16:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.

2. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.

3. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.

4. Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia.Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.

5. Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi?

6. Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu.

7. Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

8. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.

9. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;

Kusoma sura kamili Yn. 16