Agano la Kale

Agano Jipya

Yn. 13:14-26 Swahili Union Version (SUV)

14. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.

15. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

16. Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.

17. Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.

18. Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa,Aliyekula chakula changuAmeniinulia kisigino chake.

19. Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye.

20. Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu ye yote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenipeleka.

21. Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.

22. Wanafunzi wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye.

23. Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.

24. Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?

25. Basi yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?

26. Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.

Kusoma sura kamili Yn. 13