Agano la Kale

Agano Jipya

Yn. 1:1-12 Swahili Union Version (SUV)

1. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

2. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

4. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

5. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

6. Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.

7. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.

8. Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.

9. Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.

10. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.

11. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

12. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Kusoma sura kamili Yn. 1