Agano la Kale

Agano Jipya

Ufu. 7:7-14 Swahili Union Version (SUV)

7. Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.

8. Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu.Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.

9. Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;

10. wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.

11. Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,

12. wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.

13. Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?

14. Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.

Kusoma sura kamili Ufu. 7