Agano la Kale

Agano Jipya

Gal. 5:5-17 Swahili Union Version (SUV)

5. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.

6. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

7. Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli?

8. Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi.

9. Chachu kidogo huchachua donge zima.

10. Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote.

11. Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika!

12. Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!

13. Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.

14. Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.

15. Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.

16. Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

17. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

Kusoma sura kamili Gal. 5