Agano la Kale

Agano Jipya

Gal. 5:20-26 Swahili Union Version (SUV)

20. ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21. husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

22. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

23. upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

24. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

25. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

26. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.

Kusoma sura kamili Gal. 5