Agano la Kale

Agano Jipya

Gal. 4:21-30 Swahili Union Version (SUV)

21. Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria?

22. Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.

23. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.

24. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.

25. Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.

26. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.

27. Kwa maana imeandikwa,Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa;Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu;Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengiKuliko wa huyo aliye na mume.

28. Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.

29. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.

30. Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.

Kusoma sura kamili Gal. 4