Agano la Kale

Agano Jipya

Gal. 4:16-27 Swahili Union Version (SUV)

16. Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli?

17. Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa njia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku.

18. Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu.

19. Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;

20. laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu.

21. Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria?

22. Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.

23. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.

24. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.

25. Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.

26. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.

27. Kwa maana imeandikwa,Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa;Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu;Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengiKuliko wa huyo aliye na mume.

Kusoma sura kamili Gal. 4