Agano la Kale

Agano Jipya

Gal. 1:13-21 Swahili Union Version (SUV)

13. Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu.

14. Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.

15. Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,

16. alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;

17. wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski.

18. Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano.

19. Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana.

20. Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo.

21. Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia.

Kusoma sura kamili Gal. 1