Agano la Kale

Agano Jipya

Ebr. 2:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.

2. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,

3. sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

4. Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

5. Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema,

6. Mwanadamu ni nini hata umkumbuke,Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?

7. Umemfanya mdogo punde kuliko malaika,Umemvika taji ya utukufu na heshima,Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;

Kusoma sura kamili Ebr. 2