Agano la Kale

Agano Jipya

Ebr. 10:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.

2. Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?

3. Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.

4. Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

5. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,Dhabihu na toleo hukutaka,Lakini mwili uliniwekea tayari;

6. Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;

7. Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa)Niyafanye mapenzi yako, Mungu.

8. Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),

9. ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.

Kusoma sura kamili Ebr. 10