Agano la Kale

Agano Jipya

Zekaria 9:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kauli ya Mwenyezi-Mungu:Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadrakibali pia dhidi ya Damasko.Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu,kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli.

2. Hali kadhalika mji wa Hamathi unaopakana na Hadraki;na hata miji ya Tiro na Sidoniingawaje yajiona kuwa na hekima sana.

3. Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa,umejirundikia fedha kama vumbi,na dhahabu kama takataka barabarani.

4. Lakini Bwana ataichukua mali yake yote,utajiri wake atautumbukiza baharini,na kuuteketeza mji huo kwa moto.

5. Mji wa Ashkeloni utaona hayo na kuogopa,nao mji wa Gaza utagaagaa kwa uchungu;hata Ekroni, maana tumaini lake litatoweka.Mji wa Gaza utapoteza mfalme wake,nao Ashkeloni hautakaliwa na watu.

6. Mji wa Ashdodi utakaliwa na machotara.Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kiburi cha Filistia nitakikomesha.

7. Nitawakomesha kula nyama yenye damu,na chakula ambacho ni chukizo.Mabaki watakuwa mali yangu,kama ukoo mmoja katika Yuda.Watu wa Ekroni watakuwa kama Wayebusi.

8. Mimi mwenyewe nitailinda nchi yangu,nitazuia majeshi yasipitepite humo.Hakuna mtu atakayewadhulumu tena watu wangu,maana, kwa macho yangu mwenyewe,nimeona jinsi walivyoteseka.”

Kusoma sura kamili Zekaria 9