Agano la Kale

Agano Jipya

Zekaria 11:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Ziweke katika hazina ya hekalu.” Mshahara huo ulikuwa ni malipo halali kwa kazi yangu. Hivyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha, nikazitia katika hazina ya hekalu la Mwenyezi-Mungu.

14. Kisha nikaivunja ile fimbo yangu ya pili niliyoiita “Umoja;” na hivyo nikauvunja umoja kati ya Yuda na Israeli.

15. Mwenyezi-Mungu akaniambia tena, “Jifanye tena mchungaji, lakini safari hii uwe kama mchungaji mbaya!

16. Maana nitaleta nchini mchungaji asiyemjali kondoo anayeangamia, au kumtafuta kondoo anayetangatanga, au kumtibu aliyejeruhiwa wala kumlisha aliye hai: Bali atakula wale kondoo wanono, hata kwato zao.

17. “Ole wake mchungaji mbaya,ambaye anawaacha kondoo wake!Upanga na uukate mkono wake,na jicho lake la kulia na ling'olewe!Mkono wake na udhoofike,jicho lake la kulia na lipofuke.”

Kusoma sura kamili Zekaria 11