Agano la Kale

Agano Jipya

Zekaria 11:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Fungua milango yako, ewe Lebanoniili moto uiteketeze mierezi yako!

2. Ombolezeni, enyi misunobari,kwa kuwa mierezi imeteketea.Miti hiyo mitukufu imeharibiwa!Enyi mialoni ya Bashani, ombolezeni,kwa kuwa msitu mnene umekatwa!

3. Sikia maombolezo ya watawala!Fahari yao imeharibiwa!Sikia ngurumo za simba!Pori la mto Yordani limeharibiwa!

4. Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, alisema hivi: “Jifanye mchungaji wa kondoo waendao kuchinjwa.

5. Wanunuzi wao wanawachinja lakini hawaadhibiwi; na wauzaji wao wanasema, ‘Na ashukuriwe Mwenyezi-Mungu! Sasa tumetajirika’. Hata wachungaji wenyewe hawawaonei huruma.

6. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema kwamba, sitawahurumia tena wakazi wa dunia. Nitamwacha kila mtu mikononi mwa mwenzake, na kila raia mikononi mwa mfalme wake. Nao wataiangamiza dunia, nami sitamwokoa yeyote mikononi mwao.”

7. Basi, nikawa mchungaji wa kondoo waliokuwa wanakwenda kuchinjwa, kwani niliajiriwa na wale waliofanya biashara ya kondoo. Nikachukua fimbo mbili: Moja nikaiita “Fadhili,” na nyingine nikaiita “Umoja,” nikaenda kuchunga kondoo.

Kusoma sura kamili Zekaria 11