Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 9:16-20 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Mwenyezi-Mungu amejionesha alivyo;ametekeleza hukumu.Watu waovu wamenaswa kwa matendo yao wenyewe.

17. Waovu wataishia kuzimu;naam, mataifa yote yanayomsahau Mungu.

18. Lakini fukara hawatasahauliwa daima;tumaini la maskini halitapotea milele.

19. Inuka, ee Mwenyezi-Mungu!Usimwache binadamu ashinde.Uyakusanye mataifa mbele yako, uyahukumu.

20. Uyatie hofu, ee Mwenyezi-Mungu,watu wa mataifa watambue kuwa wao ni watu tu!

Kusoma sura kamili Zaburi 9