Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 7:12-17 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Watu wasipoongoka,Mungu atanoa upanga wake;atavuta upinde wake na kulenga shabaha.

13. Atatayarisha silaha zake za hatari,na kuipasha moto mishale yake.

14. Tazama! Mtu mbaya hutunga uovu,hujaa uharibifuna kuzaa udanganyifu.

15. Huchimba shimo, akalifukua,kisha hutumbukia humo yeye mwenyewe.

16. Uharibifu wake utamrudia yeye mwenyewe;ukatili wake utamwangukia yeye binafsi.

17. Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwani ni mwema;nitaimba sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu.

Kusoma sura kamili Zaburi 7