Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 7:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, nakimbilia usalama kwako;uniokoe na wote wanaonidhulumu, unisalimishe.

2. La sivyo, watakuja kunirarua kama simba,wakanivutia mbali, pasiwe na wa kuniokoa.

3. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu!Kama nimetenda moja ya mambo haya:Kama nimechafua mikono yangu kwa ubaya,

4. kama nimemlipa rafiki yangu mabaya badala ya mema,au nimemshambulia adui yangu bila sababu,

5. basi, adui na anifuatie na kunikamata;ayakanyage maisha yangu;na kuniulia mbali.

6. Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako,uikabili ghadhabu ya maadui zangu.Inuka, ee Mungu wangu,wewe umeamuru haki ifanyike.

7. Uyakusanye mataifa kandokando yako,nawe uyatawale kutoka juu.

8. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wayahukumu mataifa;unihukumu kadiri ya uadilifu wangu,kulingana na huo unyofu wangu.

9. Uukomeshe uovu wa watu wabaya,uwaimarishe watu walio wema,ee Mungu uliye mwadilifu,uzijuaye siri za mioyo na fikira za watu.

10. Mungu ndiye ngao yangu;yeye huwaokoa wanyofu wa moyo.

11. Mungu ni hakimu wa haki;kila siku hulaumu maovu.

12. Watu wasipoongoka,Mungu atanoa upanga wake;atavuta upinde wake na kulenga shabaha.

13. Atatayarisha silaha zake za hatari,na kuipasha moto mishale yake.

14. Tazama! Mtu mbaya hutunga uovu,hujaa uharibifuna kuzaa udanganyifu.

Kusoma sura kamili Zaburi 7